Sunday, September 25, 2016
Genk ya Samatta yapiga mtu 4-0
BAADA ya kupokea vipigo vitatu mfululizo, hatimaye kikosi cha Genk kinachoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji, anachocheza Mtanzania, Mbwana Samatta, kimefufuka na kuifunga Eandracht Aalst.
Kikosi hicho kiliibuka na ushindi wa mabao 4-0 mchezo wa Kombe la Ligi ambao hata hivyo Samatta hakuwepo kutokana na maumivu ya goti yanayomkabili.
Mpaka sasa nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, amekosa michezo miwili kutokana na majeraha hayo akianza na ile wa Ligi Kuu nchini humo dhidi ya Anderlecht na huo wa juzi wa Kombe la Ligi dhidi ya Eandracht Aalst.
Mtanzania huyo pia anatarajiwa kukosa mchezo mwingine wa Ligi Kuu nchini humo kesho dhidi ya Kortijk ugenini ambao ni muhimu sana kwa kikosi hicho kushinda ili kujiongezea pointi.
Genk wamemsajili Samatta akitokea kwa waliokuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika, TP Mazembe ya Congo na amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi hicho kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
bab