Friday, September 30, 2016

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amehamia rasmi mji wa Dodoma leo Ijumaa. Majaliwa aliwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma mwendo wa saa jioni akiandamana na mkewe, ambapo alipokelewa na viongozi kadha wa serikali Majaliwa aliondoka mji wa Dar es Salaam ulio umbali wa kilomita 450 mashariki. Hatua hiyo ndiyo ya kwanza ya serikali ya Tanzania kuhamia mji wa Dodoma. Kwa muda wa miezi miwili iliyopita ofisi za serikali zimekuwa zikihamishwa kwenda mji wa Dodoma. Rais wa Tanzania John Magufuli alitoa amri mwezi Julai wakati alishika wadhifa wa mwenyekiti wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi. Shughuli hiyo ya kuhama inatarajiwa kuchukua miaka mitanio na kugharimu dola milioni 500. Dodoma ulitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania na rais mwanzilishi Julius Nyerere mwaka 1973.

Rwanda yanunua ndege ya kisasa ya Airbus

Shirika la ndege la Rwanda, Rwandair, limezidisha ushindani katika uchukuzi wa ndege Afrika Mashariki na Kati kwa kununua ndege aina ya Airbus A300-200. Ndege hiyo itawezesha shirika hilo kufika masoko ya Ulaya na bara Asia. Ndege hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa kimataifa wa Kanombe, Kigali. Tanzania yanunua ndege zake mbili Ndege ndefu zaidi duniani yapata ajali Mkuu wa shirika la Rwandair John Mirenge amewaambia waandishi wa habari kuwa ndege hiyo yenye nafasi ya abiria 244 ndiyo ya kwanza katika ukanda huu na ina teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu. "Ukiwa angani ndani ya ndege hii unaweza kupiga simu, kupata ujumbe wako wa simu, ujumbe wa barua pepe, ujumbe wa WhatsApp na mawasiliano mengine. Haya hayakuwepo katika ndege nyingine tulizo nazo," amesema. "Hata katika ukanda huu na kwingineko barani afrika hakuna shirika lenye ndege iliyo na uwezo huo." Ni ndege iliyotengenezwa nchini Ufaransa na kununuliwa kwa kitita cha dolla milioni 200 za marekani. Bw Mirenge, anasema safari za shirika la ndege la Rwandair zilikuwa zinajikita sana Afrika magharibi na kati na kwamba ndege hii sasa inakuja kuongeza uwezo wa kuvamia masoko ya Ulaya, Asia na kusini mwa Afrika. Safari ya kwanza ya ndege hiyo inatarajiwa kufanyika wikendi ijayo tarehe 8 kuelekea mjini Dubai. Shirika hilo sasa linalenga kusafirisha abiria laki 750 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017.

Wednesday, September 28, 2016

Al-Shabab latoa video ya mwanajeshi wa Uganda

Kundi la wapiganaji wa al-shabab limetoa kanda ya video inayoonyesha kile inachosema ni mwanajeshi wa Uganda aliyekamatwa mwaka mmoja uliopita nchini Somalia. Katika video hiyo ya dakika sita ,mtu mmoja aliyevaa magwanda ya jeshi la Uganda anamtaka rais wa Uganda kumsaidia kuachiliwa huru. Anasema alikamatwa katika uvamizi wa kundi la al-Shabab katika kambi ya majeshi ya Afrika katika mji wa Janale,ambapo anasema kwamba kati ya wanajeshi 40 hadi 50 waliuawa. Kiongozi wa jeshi la Uganda amesema kuwa hajaona kanda hiyo,na wanatumia kila njia kuhakikisha kuwa mwanajeshi huyo ameachiliwa.

Matokeo ya mechi za ligi ya mabingwa Ulaya

Leicester city wakicheza katika dimba lao la king power wameibuka na ushindi wa pili katika michuano ya ulaya kwa kuichapa FC Porto kwa bao 1-0. Real madrid wakicheza ugenini katika dimba la Signal iduna Park wametosha nguvu na wenyeji Borrusia Dortmund kwa kufunga mabao 2-2. Nao Monaco wakavutwa shati nyumbani kwa sare ya bao 1-1 na Bayer Leverkusen. Wareno wa Sporting Lisbon wamewalaza Legia Warszawa toka Poland kwa mabao 2-0 FC Copenhagen wameibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Club Brugge Vibibi vizee wa Turin Juventus wameibuka na ushindi ugenini kwa kuichapa Dinamo Zagreb mabao 4-0,Sevilla wameshinda 1-0 dhidi ya Lyon huku Tottenham ikichomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji CSKA Moscow.

Kijana aumwa tena na buibui uumeni Australia

Mwanamume wa umri wa miaka 21 nchini Australia ameumwa tena na buibui mwenye sumu kali uumeni. Alikuwa anaenda haja katika eneo ambalo ujenzi umekuwa ukiendelea Jumanne mjini Sydney alipoumwa karibu pahala sawa na alipoumwa miezi mitano iliyopita. Jordan, ambaye hakutana kufichua jina lake la ukoo, alisema aliumwa karibu eneo sawa na aliloumwa awali. "Nafikiri mimi ndiye mtu mwenye mkosi zaidi nchini kwa sasa," aliambia BBC. "Nilikuwa nimeketi chooni nikiendelea na shughuli zangu nilipohisi uchungu wa ghafla kama niliouhisi wakati ule. Sikuamini kwamba limefanyika tena. Niliangalia chini na nikaona miguu kadha imechomoza." Kijana aumwa na buibui sehemu za siri Australia Nyoka atafuta 'joto' kwenye kiatu Amesema tangu alipoumwa mara ya kwanza, amekuwa akihofia sana kutumia vyoo vya muda. "Baada ya kisa hicho cha kwanza, kusema kweli sikutaka kuvitumia tena," anasema. "Vyoo huoshwa siku hiyo na nilifikiria ilikuwa wakati mwafaka kwangu kuvitumia. Niliangalia vyema chini kabla ya kuketi kuanza shughuli yangu. Kushtukia, mimi huyo naumwa tena." Mwenzake alimkimbiza hospitali ya Blacktown. Alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani lakini kuna uwezekano kwamba huenda asitumie vyoo vya muda tena. Mtu anapoumwa na buibui hupata maumivu makali, kutokwa na jasho na pia kupata kichefuchefu. Ingawa kumewahi kuripotiwa visa vya watu kufariki baada ya kuumwa na buibui aina ya redback, hakuna aliyefariki tangu kugunduliwa kwa dawa ya kumaliza sumu mwaka 1956.

Big Sam abwaga manyanga England

Kocha wa timu ya taifa ya England Sam Allardyce, ama Big Sam, ameachia ngazi kuendelea kuinoa timu hiyo timu ya taifa. Kung'atuka huku, kumesemwa ni kwa makubaliano ya pande mbili, na kumekuja baada ya Gazeti la Uingereza la The Daily Telegraph,kudai kocha huyo alizungumzia njia zisizo halali za umiliki wa upande wa tatu kwa wachezaji. Gazeti hilo limechapisha habari kuwa kuna maripota waliojifanya wafanyabiashara walizungumza na Kocha huyo na yeye alikiri inawezekana kuizunguka Sheria ya Chama cha Soka England, ya mwaka 2008 ya kuzuia Mchezaji kuwa na mmiliki mwingine wa Kibiashara mbali ya Klabu yake. Big Sam amekua kocha wa timu ya taifa kwa siku 67 na kuingoza katika mchezo mmoja tu, chama cha soka cha England FA imetamka Gareth Southgate kuwa kocha wa muda wa kikosi cha nchi hiyo

Tuesday, September 27, 2016

Rais wa zamani wa Israel Shimon Peres afariki dunia

Waziri mkuu wa zamani wa Israel aliyewahi kuhudumu pia kama rais Shimon Peres amefariki dunia akiwa na miaka 93. Aliugua kiharusi wiki mbili zilizopita na hali yake ikawa mbaya zaidi ghafla Jumanne. Bw Peres, ambaye alikuwa mmoja wa waliosalia kutoka kwenye kizazi cha wanasiasa waliokuwepo wakati wa kuundwa kwa taifa la Israel mwaka 1948, alihudumu kama waziri mkuu wa nchi hiyo mara mbili na mara moja kama rais. Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1994 kwa mchango wake katika mashauriano yaliyopelekea kutiwa saini kwa mkataba wa amani kati ya Israel na Palestina mwaka mmoja awali. Wakati mmoja, aliwahi kusema kwamba Wapalestina ndio "majirani wa karibu zaidi" wa Waisraeli na wanaweza kuwa "marafiki wa karibu zaidi". Bw Peres amefariki akitibiwa katika hospitali moja iliyopo karibu na mji wa Tel Aviv mapema Jumatano, jamaa zake wa karibu wakiwa karibu naye. Alikuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Sheba Medical Centre baada ya kupatwa na kiharusi 13 Septemba. Rais wa Marekani Barack Obama amemweleza Bw Peres kama "rafiki wa karibu" kwenye taarifa, na akasema: "Aliongozwa na maono ya heshima na utu na alifahamu kwamba watu wenye nia njema wanaweza kustawi pamoja." Bw Peres alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa pamoja na Waziri Mkuu Yitzhak Rabin, ambaye baadaye aliuawa, na Kiongozi wa Wapalestina Yasser Arafat. Shimon Peres alikuwa nani? Alizaliwa 1923 Wisniew, Poland, eneo ambalo sasa hufahamika kama Vishneva, Belarus Alichaguliwa kwenye Knesset (Bunge la Israel) mara ya kwanza mwaka 1959 Alihudumu katika serikali 12, mara moja kama rais na mara mbili kama waziri mkuu. Alitazamwa kama mpenda vita miaka yake ya awali - aliongoza mashauriano ya kuitafutia silaha Israel ilipokuwa bado taifa changa Alikuwa kwenye serikali iliyoidhinisha sera ya kujengwa kwa makazi ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina yaliyotekwa na Israel Hata hivyo, alitekeleza mchango muhimu katika kupatikana kwa Mkataba wa Amani wa Oslo, mkataba wa kwanza kati ya Israel na Wapalestina, uliosema wangefanya juhudi "kuishi kwa amani pamoja". Mwanzoni mwa maisha yake kisiasa, alipewa jukumu la kusimamia wanajeshi na ununuzi wa silaha za kutumiwa na Haganah, jeshi la Israel. Aliingia kwenye mkataba na Ufaransa wa kuipa Israel ndege za kivita aina ya Mirage. Aidha, alisaidia kuanzisha kiwanda cha siri cha nyuklia cha Israel. Alikuwa waziri wa ulinzi mwaka 1976, watekaji nyara kutoka Palestina walipoteka ndege ya Israel na kuielekeza hadi Entebbe, Uganda. Aliongoza juhudi za kuwaokoa zaidi ya mateka 100. Zamani alitetea makao ya walowezi wa Kiyahudi Ukindo wa Magharibi lakini baadaye akageuka mtetezi mkuu wa amani. Mara nyingi, alizungumzia haja ya kutokuwa na msimamo mgumu kuhusu maeneo ya ardhi ya Wapalestina. Aliendelea kutekeleza shughuli nyingi za umma uzeeni, kupitia shirika lake lisilo la kiserikali la Peres Centre for Peace, ambalo hutetea uhusiano wa karibu baina ya Waisrael na Wapalestina. Mwaka 2013 alisema: "Hakuna mbadala wa amani. Hakuna maana ya kwenda vitani." Alistaafu kutoka wadhifa wake kama rais mwaka 2014.

Trump na Clinton walumbana kwenye mdahalo Marekani

Wagombea urais nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wamepambana vikali katika mdahalo wa kwanza wa televisheni ambapo wamepingana katika masuala mbali mbali ikiwemo masuala ya sera, kodi, ajira na uchumi. Kadhalika wamejibizana kuhusu Vita vya Iraq na juhudi za kukabiliana na kundi linalojiita Islamic State. Msimamizi wa mdahalo huo Lester Holt amemwuliza mgombea wa chama cha Republican Donald Trump mbona kufikia sasa bado hajaweza wazi taarifa zake za ulipaji kodi. Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amemshutumu mpinzani huyo wake akisema amekuwa akikwepa kulipa kodi na kudokeza kwamba hilo lina maana kwamba hakuwezi kuwa na wanajeshi, pesa za kulipa wanajeshi waliostaafu pamoja na kufadhili elimu na huduma ya afya. Lakini tajiri huyo kutoka New York amejibu kwa kusema kwamba atatoa hadharani taarifa hizo iwapo Bi Clinton naye atakubali kutoa barua pepe 33,000 ambazo zilifutwa kutoka kwa sava yake wakati wa uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba alitumia barua pepe ya kibinafsi kwa kazi rasmi alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani. Msema kweli: Mdahalo wa Clinton na Trump Trump asema uzani wake umezidi kiwango Bi Clinton amekubali lawama kuhusu kosa hilo na kusema hakuwezi kuwa na "kisingizio". Kadhalika, Bw Trump amemlaumu mpinzani huyo wake kuhusu kupotea kwa ajira akisema nafasi za kazi "zinaikimbia nchi" na akalaumu mikataba duni ya kibiashara. Amesema Bi Clinton amekuwa mtu wa "maneno mengi, bila vitendo". Bi Clinton ameahidi kuongeza uwekezaji na kuahidi kuunda nafasi takriban 10 milioni za kazi. Mdahalo huo ulioandaliwa jijini New York huenda ukawa mdahala uliotazamwa na watu wengi zaidi katika historia ambapo watu 100 milioni inakadiriwa walitazama mdahalo huo. Kura za maoni zinaonyesha wawili hao wanakaribiana sana katika uungwaji mkono. Mambo mengine makuu yaliyoibuka kwenye madahalo: "Umekuwa ukikabiliana na ISIS maisha yako yote,'' Bw Trump amemkejeli Bi Clinton Amesema Bi Clinton hana uwezo wa kikudhibiti ukali wa kumuwezesha kuwa rais. Wamarekani Weusi wanaishi "katika jehanamu" nchini Marekani, Trump amesema, kwa sababu maisha yao yamekuwa hatari sana. Akijibu kupigwa risasi kwa watu weusi, bw Trump amesema suluhu ni kurejesha utawala wa sheria. Bi Clinton amesema akichaguliwa kuwa rais atatekeleza mageuzi katika mfumo wa sheria kwa sababu "suala la asili limekuwa likiamua mengi

Monday, September 26, 2016

Magazetini Leo Septemba 27

Tyson huenda asipigane tena

Bingwa wa uzani mzito duniani Tyson Fury huenda asipigane tena ,kulingana na afisa wa mauzo katika ndondi ya kulipwa nchini Uingereza. Fury mwenye umri wa miaka 28 amejiondoa katika pigano la marudiano kati yake na Wladimir Klitschko lililotarajiwa kufanyika Oktoba 29 kutokana na matatizo ya kiafya . Muingereza huyo ambaye hajapigana tangu kumshinda Klitschko mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita aliahirisha mechi hiyo mnamo mwezi Juni. "Fury atapokonywa mataji yake na baada ya makabiiano ya kisheria mahakamani, atasema ''sitaki tena'' ,alisema Hearn. ''Itakuwa makabiliano makubwa na itachukua mwaka mmoja kutatua.Najua kuna maswala nyeti kuhusu afya yake lakini hii ni biashara''. ''Bodi zinazosimamia mataji hayo zimetoshekwa.Ukanda wa uzani mzito duniani ni biashara yao kubwa na hawajapata fedha zozote kutokana na ukanda huo mwaka mmoja sasa''.

Kampuni ya Israel inayoweza kudukua simu yoyote

Kampuni moja ya Israel inayowasaidia polisi kudukua simu za washukiwa wa uhalifu nchini Israel Cellebrite, imesema kuwa inaweza kudukua simu yoyote aina ya smartphone. Kampuni hiyo iligonga vichwa vya habari mapema mwaka huu wakati ilipodaiwa kuwasaidia maafisa wa ujasusi nchini Marekani FBI kudukua simu aina ya Iphone iliotumiwa na muuaji wa San Bernardino. Cellebrite sasa imeieleza BBC kwamba inaweza kuingia katika simu yoyote ya smartphone. Lakini imekataa kusema iwapo inasambaza teknolojia hiyo kwa serikali za kiimla. Wiki iliopita kampuni hiyo ilialikwa katika hoteli ambayo maafisa wa polisi kutoka kote nchini Uingereza walionyeshwa vifaa na programu zinazoweza kutoa data ya simu za wahalifu

Boko Haram wawaua wanajeshi wa Chad

Wanajeshi wanne wa Chad wameuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kundi la wanamgambo wa Boko Haram kushambulia kambi yao eneo la kaskazini la mpaka na Niger mwishoni mwa wiki. Nao wanamgambo saba waliuawa wakati jeshi lilijibu shambulizi hilo. Mwaka uliopita Chad ilijiunga kwenye vita dhidi ya Boko Haram amboa walianzisha harakati zao Kaskazini Masharikia mwa Nigeria mwaka 2009. Washambuliaji wa kike wa kujitolea mhanga waliwaua takriban watu 23 na kuwajeruhi zaidi ya 100 katia kituo cha polisi na soko kwenye mji mkuu wa Chad Ndjamena mwezi Julai mwaka 2015.

Wabunge Yanga waifunga Simba

WABUNGE wapenzi wa Yanga jana walitoka vifua mbele baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya wenzao wa Simba katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mchezo huo pamoja na ule uliotangulia wa wasanii wa Bongo fleva dhidi ya Bongo movie, ulikuwa maalumu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Awali, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizindua mfumo wa tiketi za elektroniki kuingia Uwanja wa Taifa na kusema kuwa uko vizuri na unatakiwa kuendelea kutumika. Alisema ameridhishwa na mfumo huo na unatakiwa kutumika katika viwanja vya michezo, hasa huo wa Taifa ili kuziwezesha timu na nchi kupata mapato zaidi. Majaliwa aliyasema hayo baada ya kutumia mfumo huo wakati akiingia kushuhudia pambano la Wabunge wapenzi wa Yanga na wale wa Simba ambao walitanguliwa na pambano la wasanii wa Bongo movie na wale wa Bongo fleva. Katika mchezo wa netiboli, timu ya Bunge iliibuka na ushindi wa mabao 15-14 dhidi ya TBC huku Imelda Hango wa Bunge akifunga mabao tisa na Irene Elias wa TBC alifunga mabao 10 peke yake. Kwa upande wa soka, timu ya Bongo fleva walishinda kwa penalti 5-4 dhidi ya Bongo movie baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida wa dakika 90 wa mchezo. Wabunge wa Yanga waliandika bao la kuongoza katika dakika ya tatu lililofungwa na Sadifa Hamisi huku Mohamed Mchengerisa alifunga la pili na la tatu katika dakika ya tano na nane. Omary Mgumba aliifungia Simba bao la kwanza. Yanga walifunga bao la nne na tano katika dakika ya 25 na 28 kupitia kwa Mwigulu Nchemba. Wabunge wa Simba waliandika bao la pili katika dakika ya 39 lililofungwa kwa penalti na Godfrey Mgimwa. Kikosi cha wabunge wa Simba: William Geleja, Jaku Hashimu, Hamad Masauni, Kaizer Makame, Omari Mgumba, Godfrey Mgimwa, Paschal Haonga, Cosato Chumi, Hamis Kigwangala, Aziz Aboud na Sixtus Mapunda. Wabunge wa Yanga: Hamidu Bobali, Venance Mwamoto, Gibson Meiseyeki, Mussa Sima, Ahmed Nguali, Anthony Mavunde, Sadifa Hamis, Ali King, Mohamed Mchengerisa, Ridhwan Kikwete na Alex Ghashaza. Pambano hilo liliingiza jumla ya Sh milioni 187.

Marekani yaishutumu Urusi kuvunja mazungumzo ya amani Syria

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa, Samantha Power ameituhumu Urusi kwa kuzungumza uongo uliodhahiri kuhusu hatua yake nchini Syria. Amesema kuwa Warusi hawakushirikishwa katika kupamana na ugaidi nchi Syria. Bi Power aliliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba Urusi na Syria wanatekeleza vitendo vyote vya kimabavu dhidi ya upinzani uliopo Mashariki mwa Alepo, ndipo hapo uhalifu wa kivita unaweza kutekelezwa kwa kirahisi. Kwa upande mwengine Balozi wa Urusi, Vitaly Churkin, amewatuhumu waasi kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha vita ambayo yalishindikana ndani ya muda mchache tu. Mwakilishi wa Syria ameliambia baraza hilo la usalama kwamba jimbo lote la Alepo litarudishwa mikononi mwa serikali.

Akina dada wa Manchester City wawaadhibu dada wa Chelsea kwa bao 2-0

Akina dada wa Manchester City wameshinda kombea la ligi kuu ya wanawake kwa mara ya kwanza baada ya kuwashinda akina dada wa Chelsea kwa mabao 2-0 na kutangazwa mabingwa. Manchester City ambanao hawajashindwa walihitaji ushindi ili kuweza kuongoza. Nahodha wa Chelsea Katie Chapman aliifunga klabu yake mwenyewe baada ya kona iliyopigwa na Toni Duggan dakika 12 kabla ya mapumziko. Duggan alifunga bao la pili kwa njia ya penalti baada ya Lucy Bronze kuchezewa vibaya. Ushindi wa City uliwaweka kileleni kwa pointi 10 mbele ya Chelsea.

Ubabe wa China walazimu Japan kurusha ndege zake

Japan imesema kuwa ilirusha ndege zake hewani siku ya Jumapili baada ya ndege nane za China kupaa kati ya visiwa vya vyake. Ndege hizo zinaozodaiwa kuwa zile za kurusha mabomu,kufanya uchunguzi pamoja na ndege ya kivita ,zilipaa juu ya Miyako,kati ya Okinawa na Miyakojima. China imesema kuwa takriban ndege 40 zilihusika katika kile inachokitaja kuwa zoezi la kawaida. Ndege hizo hazikupita katika anga ya Japan,lakini hatua hiyo inaonekana kuwa maonyesho ya ubabe ya China. Hatua hiyo inajiri wiki moja baada ya Japan kusema itashiriki katika zoezi la pamoja na wanamaji wa Marekani katika bahari ya kusini mwa China. Msemaji mkuu wa Japan amesema kuwa taifa hilo linachunguza hatua hizo za China kwa karibu.
Yaliyojiri magazetini leo

Sunday, September 25, 2016

Diamond Na Zari Waendeleza Bata Zanzibar

Bata bado linaendleaa na mama watotooo... Diamond na mpenzi wake Zari Washkaji pia walikuwa wakiwapa kampani kwa karibu kabisaa Huu ni muendelezo tu wa kumpongeza mpenzi wake na mama wa mtoto wake na mwingine ambae anakuja katika siku yake ya kuzaliwa big up brother mungu akujaaliee wewe na familia yako heri zaid

Rais Magufuli Na Mkewe Washiriki Ibada Leo Jumapili, Wawa Kivutio kikubwa kanisani!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea Sakramenti Takatifu katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam wakati wa Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli akisalimia waumini katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.

FBI huenda likamchunguza Brad Pitt

Shirika la ujasusi nchini Marekani FBI linakusanya habari kuhusu kisa kimoja kunachomuhusisha nyota wa filamu Brad Pitt na wanawe walipokuwa wameabiri ndege ya kibinafsi wiki iliopita. Shirika hilo linaangazia uwezekano wa kuanzisha uchunguzi au la. Mkewe Pitt ,Angelina Jolie anataka kumpatia talaka muwewe kutokana na kile alichokitaja kuwa tofauti zisizotatulika. Jolie ametaka apewe watoto wote sita huku akimtaka jaji ampatie haki za kuwatembelea watoto hao mumewe. Shirika hilo la ujajusi liliambia BBC: Kutokana na ombi lenu kufuatia madai yaliotolewa kuhusu ndege iliokuwa ikimbeba bwana Pitt na wanawe ,FBI linaendelea kukusanya ukweli na litaamua iwapo litaanza uchunguzi au la. Pitt alitoa taarifa katika gazeti la People baada ya Jolie kuwasilisha ombi la kutaka talaka,akisema ameshtushwa na hatua hiyo na kuongezea: kitu muhimu ni maisha mazuri ya watoto wetu. ''Ninaviomba vyombo vya habari kutowahangaisha wakati huu mgumu

Trump atishia kumualika mpenzi wa zamani wa Clinton

Waswahili huwa wanusemi wanasema mfa maji....... utamalizia ndugu msomaji Donald Trump ametishia kumualika mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wa Bill Clinton akiwa kwenye ndoa na Hillary Clinton. Trump amesema atamualika Gennifer Flowers akae mbele kabisa, kwenye mjadala baina yake Trump na mpinzani wake wa kugombea urais, Hillary Clinton, hapo kesho. Bwana Trump alisema hayo, kujibu matamshi ya bilioneya anayeshindana naye, Mark Cuban ambaye alisema, kampeni ya Clinton imempa kiti cha mbele katika mjadala huo. Gennifer Flowers, mrembo wa zamani, amejibu kwenye Twitter, kwamba amepokea mualiko wa Bwana Trump. Haijulikani kama Trump atafuata tishio lake hilo au la.

MOJA KWA MOJA: Manchester United 4-1 Leicester City

16.22pm:Na mechi inakamilika hapa Manchester United ikiibuka kidedea baada ya kuicharaza Leicester City 4-1 16.17pm: Dakika za lala salama Manchester United bado iko kifua mbele hapa dhidi ya Leicester City. 16.14pm: Mata anatoka Ashley Young anaingia 16.11pm: Na Rooney sasa anaingia kwa upande wa Manchester United 16.10pm: Dakika ya 82 Manchester United 4-1 Leicester City 16.09pm: Namuona Wayne Rooney akivaa jezi ishara kwamba huenda akaingia wakati wowote kutoka sasa 16.08pm: Carrick anaingia kwa upande wa Manchester United. 16.06pm: Leicester wanajaribu kila mbinu hapa kusawazisha lakini hali si hali kipa David De Gea anapangua mkwaju mwengine wa mfungaji wa bao la kwanza wa Leicester Gray 15.55pm: Leicester wanaamka hapa baada ya Kujipatia bao la kwanza ,na sasa wachezaji wa Man United wanalazimika kurudi nyuma ili kulinda lango lao 15.47pm: Gooooooooooal Leicester wapata bao lao la kwanza hapa kupitia mchezaji Gray baada ya kuwachenga viungo wa kati wa Man United na kupiga mkwaju ambao david De Gea hakuona kitu. 15.46pm: Leicester wamenyamazishwa hapa,na United inaendelea kutawala mechi Kipindi cha pili kinaanza hapa kwa kasi huku Man United wakitaka kuongeza bao la tano dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi Leicester Na kipindi cha kwanza kinakamilika hapa Vijana wa Man United wakiwa kifua mbele. 15.12pm: Manchester United 4-0 Leicester 15.11pm: Goooooooooooal Pogba hatimaye aitikisia wavu timu yake hapa kwa mara ya kwanza baada ya kukosolewa kwa mda mrefu 15.09pm: Goaaaaaaaaaaal Manchester United wanajipatia bao ya tatu kupitia kijana Rashford hapa .Wachezaji wa Leicester wanalaumiana hapa 15.07pm: Manchester United 2-0 Leicester City 15.06pm: Gooooooooooooal ...Pogba aonana na mata vizuri hapa katika lango la Leicester kabla ya Mata kufunga bao la pili kwa niaba ya manchester United 15.02pm: Kwa kweli hawa wachezaji wa Leicester wanacheza kana kwamba tayari wamesalimu amri.kwani wamerudi nyuma na wanawacha wachezaji wa Man United kuwavamia kiholela 15.00pm: Manchester United sasa wanachukua udhibiti wa mechi hii na kusababisha hatari baada ya hatari katika lango la Leicester. 14.56pm: Manchester wanalivamia tena lango la Leicester ,Pogba achukua mpira na kumpatia pasi nzuri Ibrahimovic ,lakini anapiga mpira nje akiwa amebakia na goli. 14.55pm: Manchester United wavamia lango la Leicester hapa ,Ibrahimovic ampatia pasi muruwa Rashford ambaye alikuwa amebakia na kipa lakini anaupiga mpira unakuwa mwingi na unatoka lo.Rashford anakosa bao la wazi hap. 14.53pm: Manchester United 1-0 Leicester 14.52pm: Goooooooooooal Manchester United wanaongoza hapa baada ya Chris Smalling kufunga kona iliopigwa na Daley Blind. 14.51pm: Wanapanga mpira vizuri hawa wachezaji wa manchester United mbele ya lango la Leicester ,lakini wenye lango wanakataa. 14.49pm: Leicecter sasa wanaamka na kuanza kudhibiti mpira 14.46pm: Hatari pale katika lango la Man United baada ya kona kupigwa huku mabeki wa Mourinho wakilazimika kufanya kazi ya ziada kuwazuia washambuliaji wa Leicester. 14.45pm: Manchester United wanafanya masihara hapa na mpira unnatoka kona 14.42pm: Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Leicester City 14.40pm:Kikosi cha Manchester United 14.39pm: Pogba anatafuta mipira ya kumlisha Ibrahimovic lakini mabeki wa Leicester wako chonjo sana. 14.38pm: Mechi inaanza kwa mbwembwe hapa huku Manchester United ilio na wachezaji wa bei ya juu wakijaribu kuipita ngome ya Leicester 14.30pm: Manchester United vs Leicester City imeanza Huku mabingwa wa zamani wa ligi ya Uingereza Manchester United wakikabiliana na mabingwa wa ligi msimu uliopita Leicester City, mkufunzi wa Manchester United Jose Maourinho anasema kuwa Wayne Rooney ameathiriwa na ukosoaji aliopata baada ya ushindi wa timu ya Uingereza dhidi ya Slovakia.