Monday, September 26, 2016
Marekani yaishutumu Urusi kuvunja mazungumzo ya amani Syria
Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa, Samantha Power ameituhumu Urusi kwa kuzungumza uongo uliodhahiri kuhusu hatua yake nchini Syria.
Amesema kuwa Warusi hawakushirikishwa katika kupamana na ugaidi nchi Syria.
Bi Power aliliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba Urusi na Syria wanatekeleza vitendo vyote vya kimabavu dhidi ya upinzani uliopo Mashariki mwa Alepo, ndipo hapo uhalifu wa kivita unaweza kutekelezwa kwa kirahisi.
Kwa upande mwengine Balozi wa Urusi, Vitaly Churkin, amewatuhumu waasi kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha vita ambayo yalishindikana ndani ya muda mchache tu.
Mwakilishi wa Syria ameliambia baraza hilo la usalama kwamba jimbo lote la Alepo litarudishwa mikononi mwa serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
bab